1. ----------vcrs------------damaris
Shirika la umoja wa mataifa la
unesco limependekeza kuanzishwa kwa somo maalum litakalo toa mafunzo kuhusiana
na ukimwi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya maradhi hayo . Mradi huu
unaolenga wanafunzi katika shule za
msingi na za upili utatumika kama njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa maambukizi
ya ukimwi. Wakati huo huo viongozi wa kidini wameamua kuchukua jukumu la kutoa
elimu na mafunzo kwa waumini wao , kuhusiana na janga la ukimwi.