Mzozo wa kidiplomasia kati ya kenya
na sudan unatokota. Leo khartoum imempa balozi wa kenya nchini humo saa 72
kuondoka nchini humo, na kumuita nyumbani balozi wake mara moja. Khartoum imeghadhabishwa
na agizo la jana la mahakama kuu kuwa bashir anayesakwa na mahakama ya icc,
akikanyaga humu nchini atiwe nguvuni. Khartoum bungeni mbunge wa kirinyaga Joseph Gitari ameitaka wizara ya mambo ya nje kuwahakikishia wakenya wanaoishi
sudan kuwa wako salama kufuatia mzozo huu. Kenya amekuwa mshirika mkuu wa sudan
tangu kutoa mchango mkuu kupatikana kwa ule mkataba wa amani kati ya kusini na
kaskazini, na hatimaye sudan kusini kuwa taifa huru.
Kenya Sudan Diplomatic row Kisw
By Standard Digital
| Nov. 30, 2011