Eneo zima la kawethei lililoko eneo bunge la kangundo lipo katika hali ya kuomboleza vifo vya watu ishirini na saba waliofariki katika ajali ya barabarani huko mbooni, taswira ni kwamba kila boma eneo hilo limefiwa na lile ambalo halijafiwa linaomboleza kifo cha jirani. Mbunge wa kangundo johnston muthama ameahidi kuongoza kamati itakayosomamia gharama ya mazishi ya waliofariki. Na kama damaris kitavi anavyotuelezea, wenyeji wako na wakati mgumu kukabiliana na ukweli wa vifo vya ishirini na saba hao, wote walio na uhusiano kwa njia moja au nyingine.