Jazan house girl’s dilema
By Standard Digital
| Jun. 27, 2011
Familia moja mjini Mombasa inakoseshwa usingizi na kutojua hali ya mtoto wao msichana wa umri wa miaka ishirini na sita, ambaye anaaminika kushikwa mateka na mwajiri katika mji wa Jazan huko Uarabuni. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hawajui hali ya mwanao, ambaye mara ya mwisho walipozungumza naye, alidai hajala wala kunywa kwa siku tatu baada ya mwajiri wake kumrusha nje.