Marende, Murugi on IDPs
By Standard Digital
| May. 3, 2011
Spika wa bunge Kenneth Marende ameshutumu vikali wanaopinga juhudi za serikali kuwatafutia ardhi wakimbizi wa ndani kwa ndani. Marende amependekeza kwamba sasa serikali izingatie kuwapa makao wakimbizi hao katika mikoa yote minane ili suluhu ya kudumu ipatikane kwa wakenya hao. Wakati huo huo waziri wa miradi maalum Esther Murugi amesema kwamba kufikia mwezi wa septemba mwaka huu, serikali inalenga kuwapa makao wakimbizi wote halali.