Familia moja mjini Kakamega imeishi na hofu ya mwanao anayeaminika kuwa mikononi mwa wateka nyara nchini Somalia, yapata miaka mitatu sasa. Patrick Libole alitekwa nyara pamoja na muingereza Watson Murray, wakiwa kwenye kandarasi eneo la Juba. Kufikia sasa familia hiyo haijapokea ujumbe wowote kutoka kwa serikali kuhusiana na kisa hicho.