Kila jamii katika taifa la kenya ina mila na tamaduni zake na huwa hakukosekani masimulizi kuhusu asili ya jamii hizo. Mojawapo ya jamii zilizo na hadithi za asili yake ni jamii ya agikuyu ambapo wakikuyu wanaamini kuwa wao ni vizazi vya mzee gikuyu na mkewe mumbi na mabinti zao tisa. Ndiposa mara kwa mara tumekuwa tukihimizwa kudumisha tamaduni zetu hasa wakati huu ambapo vijana wengi wamekuwa wakipuuza mila zao na kuiga mitindo ya kigeni na hivi basi kupoteza mwelekeo