Manispaa ya kakamega inapangia kufanya ukarabati kwa uwanja wa mpira wa bukhungu. Manispaa hiyo imekadiria kutumia shilingi milioni 200 kukamilisha shughuli hiyo ambayo itaanza wakati wowote kutoka sasa. Uwanja wa bukhungu ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya ligi kuu ya western stima na timu zingine za daraja la chini katika eneo la kakamega.