Na Hassan Umar,

NAIROBI, KENYA, Harmonize a.k.a konde boy amekuwa msanii ambaye ana inspire vijana wengi wa mtaani, na kuwapa imani kwamba kila kitu kinawezekana. Amekuwa mstari wa mbele kufwata nyayo za boss wake wa zamani Diamond Platnumz, za kuinua vijana wenye vipaji kuwatoa mtaani na kuwaleta mbele ya macho na masikia ya dunia, miongoni mwa hao wasanii ambao wamepitia mkono wa Harmonize ni Ibraah   Akiwa na takriban miezi tisa kwenye game, Ibraah amekuwa msanii tajika ndani ya mda mfupi, amejizolea mashabiki kutoka Tanzania, Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla, ndani ya hii miezi tisa ametoa ngoma nyingi kali na za  utofauti, huku 'one night stand' aliyomshirikisha boss wake, Harmonize ikionekana kuwa ngoma yake kubwa, ikiwa na views 11M kwenye mtandao wa YouTube.   Ibraah a.k.a 'chinga' pia ametoa historia ya jina hilo(chinga) na kusema kwamba zamani kabla ya kufanya mziki alikuwa mchuuzi(hawker) wa nguo za mitumba, 'chinga' ikiwa ni neno linalomaanisha hawker kwa lugha ya mtaani ya Tanzania   Vile vile pia alifunguka na kusema, kabla ya kuwa signed na konde music world wide, alipata tabu sana, akielezea kwamba kuna sehemu nyingi alikoenda kuomba msaada wa muziki na wakamfuza, aliweka wazi aliwai kwenda WCB na pia Kings Music ya Alikiba lakini mwishowe akaishia Konde Music World wide

Je ni wimbo gani wa Ibraah unaoupenda?