Huku idara ya Elimu kaunti ya Kilifi ikiripoti kuongezeka kwa viwango duni vya masomo miongoni mwa wanafunzi kaunti hiyo, baadhi ya viongozi wanakashifu hatua ya serikali kupiga marufuku sherehe za mazishi maarufu kama Disco Matanga inayotajwa kuchangia mimba za mapema na matokeo duni ya mitihani.
Mwakilishi wadi ya Mtepeni Kaunti ya Kilifi Victor Mwaganda Gogo ameeleza kuwa sherehe hizo zimesaidia pakubwa katika kumaliza umasikini sawa na kuwapa vijana ajira ili kukimu mahitaji yao.
Ameutaja uongozi duni kuwa chanzo cha kusambaratika kwa elimu hasa miongoni mwa wasichana wa umri mdogo huku akitaka mikakati muafaka kuwekwa ili kukabiliana na swala hilo na wala sio kupiga marufuku Disco Matanga.
Matamshi yake yanajiri wakati ambapo serikali za kaunti eneo la Pwani na ile ya kitaifa ikitoa agizo la kusitishwa kwa sherehe hizo zinazoaminika kulemaza elimu hasa kaunti ya Kilifi na Kwale.
READ MORE
Kilifi learners benefit from Sh.8.5 million NGAAF scholarship
Mijikenda unity drive takes centre stage at Ngala memorial