Maisha ni mlima, kuna kupanda na kushuka.
Kuna wakati utaukwea mlima huu, na wakati mwingine utalazimika kushuka.
Wakati mwingine maisha yanakuwa machungu. Wakati mwingine huwa matamu kama asali. Hali huwa sawa, bila machungu yoyote.
Mara nyingi utawapata watu wakiwa wamesononekka, huku wakichukua muda mwingi kutafuta furaha maishani. Wengi hudhani kuwa furaha hununuliwa madukani kwa fedha.
Utawasikia wakisema: “Mimi nitafurahi tu wakati nitapata hiki au kile.”
Furaha ya kudumu imo ndani yako, wala sio kwa vitu vilivyoko nje ya utu wako.
Fahamu kuwa zana zote za kukupa wewe furaha hazipo mikononi mwa binadamu mwenzako, au hata kwenye kazi yako, urembo wako, watoto wako au hata wapenzi wako!
Chemichemi za furaha ya kweli ipo katika nafsi yako. Kwa hivyo sio vyema kuhangaika maishani ukitafuta watu wenye kupa furaha na kuitosheleza maisha yako.
Wewe mwenyewe ni sharti ujipe furaha kulingana na mtazamo wako wa maisha.
Wengi wamesema kuwa furaha huja pale tunapokuwa na fedha nyingi, kazi ya kifahari, urembo na kadhalika.
Je, wajua kuwa kuna warembo wengi humu duniani ambao wamejitia kitanzi kwa kukosa furaha? Je, wajua kuwa kuna matajiri ambao wameonelea ni kheri wafe kwa kukosa raha? basi ina maanisha kuwa hakuna kitakacho kupa raha iwapo hakijakita mizizi katika nafsi yako.
Ni sharti ujiite kwenye mkutano, yaani wewe kwa wewe ili ujielewe mwenyewe.
Wasiliana Nami;annnjambi@yahoo.com