Suleiman,

SUMMARY
Serikali yajitetea baada ya CAF kupokonya Kenya nafasi ya kuandaa CHAN mwakani

Serikali imejitetea baada ya Shirikisho la Soka Barani, Afrika CAF kuipokonya Kenya nafasi ya kuandaa mashindano ya CHAN Januari mwakani. Katika kikao na wanahabari, Katibu wa Wizara ya Michezo, Peter Kaberia amedai kuwa kamati ya shirikisho hilo iliipokonya Kenya nafasi hiyo kutokana na hali ya kisiasa nchini.
Kaberia amesema alifanya kikao na Rais wa Shirikisho la CAF na manaibu wake ambao walimweleza bayana kuwa mkondo wa kisiasa nchini haubashiriki hivyo kuwa vigumu kwa Kenya kupewa nafasi hiyo suala ambalo limewaghadhabisha Wakenya.
Naye Rais wa Shirikisho la Soka Nchini, FKF Nick Mwenda amesema madai ya viwanja vya michezo kutokuwa tayari hayana msingi kwani viwili vimekamilika kwa asilimia 80% huku vingine viwili vikitarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Disemba hivyo suala hilo halina uzito.
Aidha Mwenda amesema Kenya imepewa nafasi ya kuandaa mashindano ya kandanda ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 au walio chini ya umri wa maika 19 mwaka wa 2019 ambapo inakisiwa kwamba joto la kisiasa halitakuwapo nchini.
Ikumbukwe Wakenya wamelalamikia suala la Kenya kupokonywa nafasi hiyo ambayo sasa imeachwa wazi huku nchi ya Morocco na Afrika Kusini zikiwa mstari wa mbele kuchukua nafasi hiyo