Na, Stephen Mukangai
ANTHONY DANIEL MULE ndiye mwenyekiti mpya wa kilabu ya AFC leopards. Mule aliibuka mshindi kura zilizopigwa Jumamosi, Julai 24 na mashabiki 3000 waliojitokeza katika uwanja wa michezo wa Kasarani jana.
DANIEL MULE ambaye alikuwa katika serikali ya mseto ya uwongozi wa timu hiyo, aliibuka mshindi kwa jumla ya kura 1160 na kumbwaga mpinzani wake wa karibu Maurice Amahwa aliyepata kura 822.
Aliyekuwa naibu Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Robert Asembo alikuwa wa tatu kwa jumla ya kura 119.
MGOMBEZI mwengine wa kiti cha uwenyekiti Mathews Opwora alijiondoa katika kinyang’anyiro hicho.
Felix Shitsama ndiye naibu mwenyekiti. Katibu mkuu ni Oscar Igaida na atasaidiwa na Elijah Stazo. Timothy Lilumbi alichaguliwa kuwa katika mtendaji. Oliver Imbenzi ndiye mwekahazina na atasaidiwa na Justus Makabila.
Uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya amani na viongozi waliochaguliwa watahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.