Wakulima wa ngano mjini Narok wamefanya maandamano kupinga hatua ya waziri wa fedha Uhuru Kenyatta, kupunguza ushuru wa ngano na bidhaa za ngano zinazoagizwa kutoka nchi za nje, jambo lililopelekea bei ya ngano nchini kushuka. Wakulima hao wamesema kwamba hatua hiyo imepelekea wao kupata hasara kubwa, kwani awali gunia moja la ngano liliuzwa kwa shilingi elfu mbili mia nane, na sasa wanalazimika kuuza kwa shilingi elfu moja mia nane.