Fikiria kuhusu maisha yako. Picha: Hisani

Je wajua kwamba maswali unayojiuliza kimoyomoyo ndiyo yenye jawabu nyingi kuhusu mwelekeo wa maisha yako au hata mahali ambapo maisha yako yalipo sasa?

Kujiuliza maswali kulingana na mambo yanayokuathiri maishani ni jambo la busara, kwani wajua huwezi pata jibu bila kutambua swali haswa nini!

Barabara ya uhuru wako kimaisha itategemea maswali unayojiuliza. Na maswali unayojiuliza pia jibu lake ni swali, kwa hio maswali yako lazima yawe mazito. Mna minoia nata, buankuwa kuna maswali ambayo naamini ni muhimu zaidi maishani, ambaoo kila mwanadamu anapaswa kujiuliza, hususan binadamu ambao wana azma ya kutamani mafanikio katika fani mbali mbali katika maisha yao.

Hebu jibu maswali haya kwa kadiri ya uwezo wako na utaona mabadiliko makubwa , sio eti ni lazima ujibu maswali haya yote kwa wakati mmoja lakini waweza kuchukua muda mchache kila siku kuyatafakari maswali haya kabla ya kuafikia majibu.

1. Ungekuwa na nafasi ya kuanza maisha yako upya je ni kipi ungebadikisha?

2. Je maafikio au malengo yako ni yepi maishani ?

3. Je wewe unapenda kufanya nini?

4.Ungekuwa na kila kitu unavhohitaji kufaulu maishani katika kipindi cha mwaka mmoja hivi, ungeshughulikia na nini haswa!

5. Ni nini chenye kukupa kero kubwa ulimwenguni ?

6. Je unatafuta nini maishani, unatamani nini ?

Ukiyajibu maswali haya kwa undani wako na kwa mtazamo wa kufanikiwa basi nina hakika kuwa utabadilisha taswira ya maisha yako

kwani maswali haya yatakupa fursa ya kufikiria kindanindani kuhusu muelekeo wa maisha yako , na pia kukupa fursa ya kujiuliza ni nini unachofanyia muda wako , raslimali ulizo nazo , na pindi siku zinavyosonga unajiendeleza au unatudi nyuma na kuwa tu kizingiti cha watu wengine .

Nimeshawahi kuchukua muda na kujibu maswali haya amini usiamini majibu yake yalinifungua macho mno , ni maswali ambayo mimi huyajibu kila baada ya muda kwani utapata kuwa majibu yake hubadilika kila msimu

Nakutakia kila la kheri unapokunjua jamvi moyà la maisha yako kwa kupata majibu yenye manufaa kwako

Wasiliana nami

annnjambi@yahoo.Com