Na, Caren Omae
Mgomo wa madaktari uneendelea kuvutia hisia za mashirika mbalimbali, huku wito ukitolewa kwa washikadau kuweka mikakati ya kuusitisha.
Mashirika hayo yakiwamo Baraza la Kidini, Muungano wa Madaktari wa Kike na Muungano wa Utoaji Matibabu, yamesema wanaohusika wanapaswa kulegeza misimamo ya matakwa yao.
Kulingana na Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari wa Kike, Daktari Kristene Sadia, wanaougua saratani, matatizo ya figo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na mengineyo ndio wanaoathirika zaidi. Wengine ni wenye virusi vya ukimwi na waliokuwa wakihudumiwa kutokana na athari za uraibu wa dawa za kulevya.
Mashirika hayo yanasema yatawasilisha waraka kwa wanaohusika katika mazungumo hayo, kutaka mgono huo usitishwe. Wakati uo huo, yanapendekeza mazungumo hayo kuwekwa wazi kwa umma ishara ya uwazi.