Leaders mourn Michuki
By Standard Digital
| Feb. 15, 2012
Katika majengo ya Wizara ya Mazingira, upweke, na huzuni ndizo zilitanda, katika afisi yake, kiti chake na meza yake zilikuwa nadhifu, kila kitu kilipangwa vizuri, lakini zilikosa mwenyeji. michuki aliaga dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali moja hapa jijini nairobi baada ya kupata mshtuko wa moyo.michuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe humu nchini aliyehudumu katika serikali tatu, kuanzia jomo kenyatta, moi, na kibaki. Wenzake serikalini, bungeni na viongozi hapa nchini walimiminia sifa kedekede kutokana na uwajibikaji na utendakazi wake. john michuki atazikwa nyumbani kwake kangema, kaunti ya muranga, jumanne ijaayo.