Je, umewahi kujiuliza ni vipi mtu asiye na mikono anaweza kuendesha ndege? Leo hii tunamuangazia Jessica Cox ambaye ni raia wa Marekani ambaye licha ya kuwa na ulemavu wa kukosa mikono amejipiga kifua na kusomea taaluma ya urubani. Jessica amefika humu nchini ili kuwapa moyo walemavu kama yeye na kuwataka wawe ni wenye kujitegemea kwani ulemavu sio mwisho wa kufanikiwa maishani.
Handless pilot - Swahili
By Standard Digital
| Sep. 27, 2011