Mwanamume mwenye umri wa miaka 45 amefungwa jela kwa miaka 45 baada ya kukiri kosa la kumnajisi mtoto wa miaka miwili.
Mahakama imeambiwa kuwa Erasus Kariuki mwenye umri wa miaka 39, alikuwa kanisani katika eneo la Zimmerman, Kaunti ya Nairobi ambapo alimfanyia unyama huo mtoto huyo.
Akijitetea, Kariuki amemlaumu shetani kwa kumsukuma kumnajisi mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili Julai tarehe 3 mwaka huu.
Mahakama jijini Nairobi imeambiwa kuwa mshukiwa alikuwa amehudhuria hafla ya harambe kanisani humo ambapo alitoa mchango wake wa shilingi 100 kisha kumnajisi mtoto huyo kanisani.
Wakati wa tukio hilo waumini waliosikia kilio cha mtoto huyo akiwamo mamake walikimbia kumwokoa huku akikabiliwa kabla ya kuokolewa na polisi.
READ MORE
Police sound alarm over surge in defilement cases
Man linked to stealing, defiling 15-year-old girl detained pending bond ruling
75-year-old man arrested for defiling step granddaughter
Report: Low funding, slow response leave children exposed to abuse
Mtoto huyo anaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Komarock Modern Hospital.