Mamlaka ya Utozaji Kodi Nchini, KRA inalenga kukusanya shilingi bilioni 56.6 ambazo zilipotea kutokana na visa vya ukwepaji kulipa kodi.
Fedha hizo zimehusishwa na kesi 152 zilizowasilishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini tangu mwezi Julai mwaka huu.
Kipindi hicho kinaendana na wakati alipoondoka mamlakani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa KRA John Njiraini tangu mwaka 2012 na wadhifa wake kutwaaliwa na James Mburu.
Ikumbukwe kuwa wakati wa kuapishwa kwake, Mburu ambaye alikuwa akihudumu katika wadhifa wa Kamishna wa Masuala ya Ujasusi na Oparesheni katika Mamlaka hiyo, aliahidi kuwakabili wanaokwepa kulipa kodi kwa mbinu zozote zile.