Katika sehemu ya pili ya makala ya mpapatiko wa wazee tunaangazia wasiwasi wa kuwa mzee ndani ya vijiji vya kilifi. Hii ni kutokana na wazee wenye kutoa mvi au kudhihirisha ishara za uzee kutishiwa maisha na wengine kulazimika kuhama kabisa kutoka yaliyokuwa makaazi yao , kwa kuhofia kuuawa . Anne ngugi anaangazia visa vya wanawake watatu ambao wanaishi kwa wasiwasi kwa kudaiwa kuwa wachawi .