Kinyume na ilivyotarajiwa, Rais Uhuru Kenyatta amekwepa kuzungumzia suala lililochochea hisia kali la maafisa wa polisi kupungiziwa mishahara, badala yake kulenga masuala mengine yanayohusu usalama wa nchi. Akizungumza alipoongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu katika Chuo cha Mafunzo cha Kiganjo, Rais amesema mpango wa kushirikiana miongoni mwa taasisi mbalimbali wakati wa kukabili visa vya utovu wa usalama nchini, umechangia pakubwa kukabiliwa kwa tishio hilo. Amezitaja hatua zilizopigwa kuwakabili magaidi kuwa mojawapo ya mafanikio hayo. Rais amesema ana imani kuwa waliofuzu leo wataendeleza mpango huo wa serikali.
Rais aidha amewashauri kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuzingatia waliofunzwa chuoni humo katika utendakazi wao. Rais amewashauri kudumisha uhusiano mwema na raia wa maeneo watakayotumwa kuhudumu ili kuboresha sifa za idara hiyo.
Wakati uo huo amewasihi wananchi kushirikiana na vikosi vya usalama kukabili ugaidi ambao ungali tishio kuu kwa usalama wa nchi.
Aidha amesema serikali yake itaendelea kuvinunua vifaa vya kisasa na kutenga fedha za kutosha ili kuwawezesha maafisa wa polisi kuyatekeleza majukumu yao ifaavyo.
Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi, amesema ana imani kwa maafisa hao ikizingatiwa ni kundi la kwanza lililofuzu chini ya mafunzo ya mtalaa mpya.
READ MORE
Court freezes Wamatangi accounts over Sh813m graft scandal
Kenyan hotels to be classified after 10-year wait
Outcry as Migori inmate with severe burns taken to hospital two months late
Twenty-three counties facing food shortage as drought crisis deepens
Jumla ya makurutu elfu tatu mia tisa sitini na tisa wamefuzu katika hafla hiyo ambayo pia imehudhuriwa na Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinett.