Mwenyekiti wa Chama cha FORD Kenya na vilevile Mbunge wa Kwanza  Kaunti ya Trans Nzoia,  Ferdinand Wanyonyi  amemtahadharisha  Rais Uhuru Kenyatta kutofurahia na kushabikia mapema ndoa ya kisiasa baina yake na Kinara wa NASA Raila Odinga.

Kwenye kikao na wanahabari katika Shule ya Upili ya Wasicahana ya Alexernder Muge, Wanyonyi amekariri kuwa bado kuna mengi ya kusubiriwa kubaini ikiwa ndoa hiyo ya kisiasa itadumu au la.

Kadhalika Wanyonyi amekariri kuondoka kwa ODM kutavipa nguvu hata zaidi  vyama tanzu vya NASA kikiwamo kile cha Ford Kenya , ANC na Wiper kuungano na kuafikia ndoto zao za kisiasa.