Majuzi Rais Uhuru Kenyatta aliafanya ziara ya kibinafsi nyumbani kwa Rais John Pombe Magufuli mkoani Geita. Magufuli katika hotuba fupi ya kumkaribisha mwenzake alichekesha wengi aliposema kuwa alidhani kaja kumpa pole baada ya Harambee Stars kuifunga Taifa Stars 3-2 kule Misri katika michuono inayoendelea ya AFCON. “Nilipata simu ya Rais Uhuru akitaka kuja kunitembelea na nikakubali. Nilidhani kataka kunipa pole kwa Kenya kutufunga na hali tulikubaliana tuende sare 2-2. Hata hivyo nimemsamehe kwani walichapwa na Seneagl 3-0 na hali sisi tulifungwa na hao Senegal 2-0,” alitania Magufuli. Ziara ya Rais Uhuru ina umuhimu mkubwa hususan kukuza mahusiano ya nchi hizi mbili ambayo yalikuwa na uhusiano legelege.

Yamkini  matamshi ya mbunge fulani wa Kenya (jina twabana kwa ajili ya sheria) ya kuchochea kufukuzwa kwa wafanyibiashara watanzania Kenya kulilazimu Rais Uhuru kwenda haraka kutuliza hali ya uhasama iliyokuwa ikitokota. ‘Mwanasiasa huyo mwenye matamshi ya chuki si mwema na ni hatari kwa usalaam na amani’ asema Magufuli na kumshukuru Rais Uhuru kwa kuchukuwa hatua ya dharura kukarabati ufa huo ambao ulielekea kuanguka. Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa jadi kwani wakazi hapa huishi kindugu.Kuna makabila kama matano amabayo yako katika nchi hizi mbili. Makabila hayo ni Wamaasai, wakuria, wajaluo, waswahili na wadigo.

Hili pekee ni muhimu kwani huwezi kutenga kabila moja. Kuna wakenya wengi wanaoshi Tanzania na pia wabongo tele huku Kenya.Mshiakam

no huu ni muhimu kukuza na kujenga undugu kikamilifu. Dunia ya sasa inataka chumi za nchi kuunagna ili kufaulu. Sambamba kama alivyoeleza Magufuli kuwa idadi kubwa ya watu ndio njia moja ya kukuza uchumi. Magufuli alitowa mfano wa Uchina na

India walio na mamilioni ya watu kuwa wana uchumi mkubwa kwa ajili ya watu wake amabao ni soko na nguvu kazi. “Hata Ulaya inaungana na kuwa na soko kubwa la jumuiya ya ulaya.Ni

kwanini sisi katika kanda hii tusiungane?” auliza Magufuli. Mchanganuzi wa siasa kanda ya pwani Kitumbondani Bwanamake aunga mkono kauli ya Magufuli na kusisitiza umoja.

Hatahivyo, Bwanamake asema Tanzania iwe mkweli katika hatua hii na si una? ki wa kusema bila kutenda. “Magufuli lazima afunguwe biashara kwa wakenya nchini kwake vile Kenya inavyofanya na asiogope wakenya eti watameza uchumi wake,” asema Bwanamake na kumtaka Magudfuli awe na roho sa?  na Kenya.

 Mbali na kufunguwa soko kubwa la kanda hii mahusiano mema yataleta amani.Tukiwa na uhusiano mwema wa kikweli basi wakazi wa kanda watakuwa huru kufanya biashara na kukuza amani. Rais Uhuru alisema atamtuma mwanawe wa kiume Tanzania na hata ikiwezekane aowe binti wa Tanzania kujenga undugu kauli iliyokubaliwa na Magufuli.

Umoja wa kanda utaondowa umasikini kwani kutakuwa na nafasi pana ya kujiendeleza kiuchumi katika sehemu pana. “Afrika mashariki ina raslimali nyingi lakini hazijaboreshwa haswa katika Tanzania hivyo Kenya yaweza kusaidia Tanzania ku? kia ufanisi,” asema Bwanamake. Kauli hii si ngeni kwani hata baba wa taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Kamabrage Nyerere alisema Kenya inaweza kusaidia Tanzania pakubwa. Katika kipindi  cha ‘Kutoka Maktaba’ cha shirika la habari Tanzania TBC Nyerere alinukuliwa akitowa kauli hii. ‘Badala ya kwenda ulaya kufata madaktari tuvuke kwa jiarni hapa Kenya tulete madaktari wao’ asema Nyerere. Kimsingi mahusiano ya kanda ni muhimu lakini yawe ya uwazi na  ukweli si una?ki.