Rais Uhuru Kenyatta sasa analenga ushirikiano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi ili kufanikisha ajenda ya serikali kuhusu makazi ya bei nafuu.
Rais Kenyatta amesema licha ya kwamba hatua mahususi zimepigwa katika kufanikisha ajenga nne za serikali, uhaba wa makaazi unaendelea kuwa changamoto kwa serikali yake.
Akizungumza kwenye Ukumbi wa KICC wakati wa mkutano wa UN -Habitat, Rais amesema pana haja kwa wanachama wote 36 wa muungano huo kushirikiana ili kuimarisha makazi.
Rais aidha ameonesha utayarifu wa serikali kutekeleza ajenda zake nne kuu kabla ya kukamilika kwa muhula wake.
Amelalamikia ukuaji wa kasi wa mitaa ya mabanda akisema imechangia kwenye uharibifu wa mazingira nchin.
Rais Kenyatta analenga ushirikiano wa Umoja wa katika Ujenzi wa makazi
By Esther Kirong'
| May. 27, 2019