Ndege aina ya Boeing 787-8  ya Shirika la Ndege la Kenya Airways iliyozinduliwa rasmi kwa safari za moja kwa moja kutoka uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuelekea Marekani, inatarajiwa kutua katika Jiji la New York saa saba na dakika ishirini na tano adhuhuri saa za Kenya , ikiwa ni sawa na saa kumi na mbili na dakika ishirini na tano asubuhi saa za marekani.

Ndege hiyo ya moja kwa moja imerahisisha usafiri kwa kupunguza saa saba ambazo zilikuwa zikitumiwa kuunganisha ndege katika mataifa ya Uropa au Mashariki ya Kati. Kabla uzindunzi huo, safari ya kilomita 11,849 kutoka Kenya hadi Marekani ilichukua saa ishirini na mbili.

Ndege hiyo ina marubani wannne, na wahudumu wa ndege kumi na wawili.

Mwezi uliopita akiwa Marekani Rais Kenyatta alizungumzia uzinduzi huo ytakao boresha uhusiano kati ya maitaifa hayo mawili.

Ndege zitakazokuwa zikiondoka JKIA zitapaa saa tano na dakika ishirini na tano usiku saa za Kenya kila siku, na kufika Mareknai katika Uwanja wa  John F. Kennedy saa kumi na mbili na dakika ishirini na tano asubuhi saa za marekani.

Uzinduzi huo uliendelea jinsi ulivyopangwa hasa kufuafikia agizo la mahakama ambalo lilizuia mgomo wa Chama cha Wafanyakazi wa Ndege ambao ungeathiri uzinduzi wa. Mahakama ya Uajiri na Leba aidha iliwazuia wafanyakazi hao kutaka kupewa fedha zaidi iwapo watahudumu katika safari hizo.

Chama hicho kilitaka kutia saini mkataba mpya wa utendakazi kabla ya kuhudumu katika safari hizo kwani kulingana na mkataba wa sasa, wanastahili kufanya kazi kwa saa kumi na tano ambapo sasa watalazimika kufanya kazi saa tatu zaidi.