Ushindi wa Wambora wabatilishwa
By
| Feb. 22, 2018
Ushindi wa Wambora wabatilishwa
Caren Omae
Mahakama Kuu ya Embu imebatilisha ushindi wa Gavana wa Embu Martin Wambora. Akitoa uamuzi huo, jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa ulikuwapo ukiukaji wa sheria za uchaguzi wakati wa shughuli ya kupigwa kwa kura hizo, hali iliyoathiri matokeo ya uchaguzi huo.
Aidha amemwagiza Wambora kulipia shulingi milioni tatu ambazo ni gharama ya kesi.
Kesi ya kupinga ushindi wa Gavana huyo iliwasilishwa na mshindani wake Lenny Kivuti.Wambora ni wa tatu kupoteza kiti chake kuafuatia uamuzi wa mahakama.?