Klabu ya Rangers leo ilisalimu amri na kukubali wageni wao, klabu ya benki ya kenya commercial kuwapa kichapo cha mabao 3-1 katika mechi ya kwanza iliyosakatwa uga wa city. Kushindwa kwa Rangers ilikuwa afueni kwa Tusker ambao walirejea uongozini baada ya kushinda mechi yao 2-1 dhidi ya City stars. Gor mahia kwa mara ya pili msimu huu walitoka sare na Mathare United.