Mashakidi Kuhojiwa CID

Idara ya polisis sasa imesema uchunguzi kuhusiana na tetesi za kuhongwa kwa mashahidi ili kutoa ushahidi bandia hautawalenga mashahidi waliojitokeza  wakidai kuhongwa peke yake, bali hata tume nzima ya KNCHR inayoshutumiwa kwa kuwahonga mashahidi ili wamlimbikizie lawama mbunge William Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi. hatua hii ya polisi inajiri baada ya majibizano makali baina ya ruto na tume hiyo ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu.