Msako Wa Changaa Bungoma

Zaidi ya lita elfu hamsini na tano za pombe haramu zimenaswa katika maeneo ya Bungoma na Kakamega na maafisa wa polisi katika operesheni kali dhidi ya upishi wa pombe haramu. La ajabu ni kuwa mizoga ya panya pamoja na vipande vya chupi za wanawake vilipatikana kwa wingi ndani ya mitungi hiyo ya busaa, kangara na chang’aa, jambo ambalo lilibua wasiwasi kwa wanaopenda kuibugia pombe hiyo. Hata hivyo baadhi ya washukiwa walifanikiwa kukwepa mtego wa polisi. Inadaiwa vifaa hivyo vya ajabu vinatumika kwa ushirikina ili kuwavutia wateja.