NASA WAWATAKA WAKENYA KUJIOKOA WENYEWE

Muungano wa NASA unaoongozwa na Mheshimiwa Raila Odinga umewaonya wakenya kwamba huu ndio wakati wa kipekee wa kujinasua kutoka kwa ulaghai wa viongozi wa chama cha Jubilee.

Akizungumza na wakenya katika mdahalo wa wagombea urais uliofanyika tarehe 24/07/2017,Bw Odinga alitumia fursa hio kujieleza na kufafanua manifesto ya NASA huku akidai kwamba ndiyo dawa pekee ya matatizo yanayoikumba nchi ya Kenya.

Ameisuta serekali iliyopo kwa kile alichodai kwamba ni kutowajibika kulingana na mahitaji ya katiba.