+ Post your Story

For Enquiries Chat with us on Whatsapp on 0712 538 802

Politics
Abduba Dida apata pigo, mahakama kuu yatupilia mbali kesi ya mjadala wa urais
By Joseph Sosi | Updated Jul 07, 2017 at 11:01 EAT
abduba-dida-apata-pigo-mahakama-kuu-yatupilia-mbali-kesi-ya-mjadala-wa-urais
Majaji katika kongamano Lao la kila mwaka Mombasa

Mahakama kuu nchini leo hii inatarajiwa kuamka hatma ya kesi mbili muhimu zinazohusu uchaguzi mkuu wa Agosti 8.

Majaji wa mahakama hiyo walioteuliwa na Jaji Mkuu David Maraga wanasubiriwa kuamua kesi kuhusu watakaoshiriki mdahalo wa urais ambao umeratibiwa kufanyika Jumatatu.

Hii ni baaada ya mwaniaji wa wa kiti cha urais katika chama cha Alliance for Real Change Abduba Dida keuelekea mahakamani akishtumu waandalizi wa mjadala huo kuwa wenye ubaguzi dhidi yake.

Kesi hiyo sasa katika uamuzi uliotangazwa leo hii imetupiliwa mbali na mahakama na kwa mujibu wa wakili wake Dida, uamuzi huo umetolewa na majaji na wamesema hawajaona aina yeyote ya ubaguzi katika maandalizi ya mjadala huo.

Mgombea huyo hajazungumzia uamuzi atakaofanya baada ya kesi hiyo kugonga mwamba. 

Majaji wa mahakama kuu wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusu lawama ya Bw Dida baadaeye leo mjini Mombasa huku wapinzani wakuu, Rais Uhuru Kenyatta na mgombea kiti hicho katika mrengo wa NASA Raila Odinga wakiwa tayari wametangaza kuwa wamejiondoa kwa kutoshirikishwa kwenye maandalizi. 

Kadhalika, majaji wana kibarua mchana huu kutoa uamuzi katikati mahakama ya Milimani kuhusu kesi inayopinga kutolewa kwa kandarasi ya uchapishaji karatasi za kupiga kura kwa kampuni ya Al Guhrair.

Muungano wa NASA uliewasilisha kesi hiyo mahakamani wakiitaka kandarasi hiyo ya tume ya IEBC kwa kampuni hiyo ifutiliwe mbali kwa madai kwamba Rais Uhuru Kenyatta alishinikiza tume hiyo kupendelea kampuni hiyo.

Uamuzi kuhusu kandarasi hiyo unasubiriwa na wengi na itakumbukwa kuwa ni siku thelathini na moja tu zimesalia ili uchaguzi mkuu kufanyika na karatasi za kupiga kura zinachapishwa na kampuni hiyo isipokua tu za urais. 

Do you have stories, videos or pictures you would like to share with the world?

Simply click on Post Your Story button placed at the top of the website


This is a citizen journalism website. The views expressed here do not represent that of the Standard Group Ltd. Read the terms and conditions
COMMENTS
Latest Stories
Popular Stories
Featured Sections
More From This Author
Top Contibutors