Skip to main content
× THE NAIROBIAN POLITICS TEN THINGS ASIAN ARENA TRAVEL FEATURES NAIROBIAN SHOP MONEY FASHION FLASH BACK HEALTH UNCLE TED BETTING Podcasts E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×
SPORTS

Ganga yajayo: Kuteleza katika mapenzi si kufeli, jaribu tena baadae

BLOGS
By Stephen Mburu | August 26th 2021

Kuteleza si kuanguka bali ni kusonga mbele. Hii ni kauli ambayo walishaisema wazee wa zama zile. Kauli hii kila ninapoitafakari huniletea taswira tofauti tofauti.

Kwanza, kunai le taswira kwamba unapotembea ukielekea shughuli zako na upatane na chombo au kitu kilichopo chini ukigonge kwa bahati mbaya. Hutaanguka moja kwa moja. Utateleza, usonge mbele.

Vile vile, unapopatana na unyevuunyevu kwenye sakafu bila kutarajia na ukanyage vibaya, utataleza pia! Utasonga mbele huku kasi yako ya kutembea ikiongezeka. Utakuwa fikra zako zilizokuwa mbali zimeregeshwa kwa sehemu ile.

Halikadhalika, mawazo yako yote yataanza kufikiria kuhusu jinsi ya kujistawisha na kuhakikisha kwamba hatari iliyojitojeza unahimili na kuituliza ili isije ukakuathiri tena.

Taswira ya pili nayo hunijia kwa njia hii- kwamba hata tunapofeli maishani, huwa hatusalii tulipokuwa kabla ya kufeli. Huwa tunasonga mbele hatua kadhaa.

Kwa mfano, unapojaribu kuwekeza katika biashara kisha hatimaye iporomoke. Hutasalia ulipokuwa, utaondoka na somo kubwa kuhusu mambo ambayo hayafai katika baishara. Japokuwa hutaondoka na hela au faidam utaondoka na somo.

Somo ambalo ukilitumia vyema keshoye utakula vinono na hata ubakishie wengine. Huo ndio ukweli wa maisha haya ambayo tunaishi.

Si katika biashara tu, tuwaze pia kuhusu masomo. Wengi wasiopasi mitihani yao huangalia nyuma na kusema kwamba heri wasingeenda chuoni bali swali kuu ni je, mambo waliojifunza shuleni yakiwemo ya kupendana, kujali wengine na kuheshimu watu wangeyajulia wapi iwapo si huko?

Hapo ndipo tusemapo kwamba kuteleza walikoteleza hakufai kamwe kuwa kigezo cha kuangaziwa katika maisha yao ya usoni bali inafaa kuonekana kama funzo. Funzo walilojifunza watu hawa.

Yamkini asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Ulimwengu huu uliona kucha kubwa na usiofunza kwa huruma ndio utakaowafunza watu hawa.

Kila tunapowaza kuhusu kuteleza lazima tutoe suluhu. Suluhu ya mawimbi ambayo humkumba mtu. Kwa mfano iwapo mzazi alitarajia mwanawe angepita mitihani ya kitaifa ili aende kwenye chuo kikuu azamie kozi kama za rubani au udaktari, ila maazimio kama haya yashapitwa na muda, endapo mwanawe atashindwa kupita hafai kulaumiwa.

Mtoto huyu aliyejaribu kadri ya uwezo wake anafaa kupongezwa. Apewe shukran zake za dhati kwa kujaribu awezalo ila akumbushwe kwamba mikononi mwa mamaye kulikuwa kwema ila mikononi mwa dunia hakuna huruma.

Kikuu zaidi ni kwamba aliteleza, hakuanguka! Atakapostawi ahakikishe kwamba harudii makosa aliyoyafanya mwanzoni. Mwisho wa siku ni kosa kubwa sana kurudia kosa lile lile alilolifanya wakati uliopita.

Ipo haja kubwa sana endapo watu watajifunza kuhusu jinsi ya kukwepa masaibu wanayoyapitia na jinsi ya kuondokea masaibu haya kwa njia ifaayo. Hakika, ukuu wa jambo si kufaulu tu bali kisa na misingi wa jambo lenyewe.

Kwa upande mwingine, vijana wengi ambao wamepitia masaibu ya mapenzi- waliteleza. Hawakuanguka. Waliteleza ila nafsi zao zimekataa kamwe kuachilia uchungu huu. Nafsi zao zimesalia zikiwaza kuhusu makovu yaliyokwama mioyoni mwao.

Hili ni kosa na si kosa tu bali kosa nzito mno kwani walipoteleza wao walibaki pale pale kwenye unyevu. Hawakusonga mbele ilhali ni falsafa ya maisha kwamba jambo linapotekea leo, jifunze nalo kisha usonge mbele.

Hamna haja matukio ya kale yakuangamize au hata yaangamize ndoto zako za kesho za kuwa na familia yenye furaha na yenye ucheshi tele.

Naam, mapenzi ni taabu kwa vijana wengi kutokana na hali ya kujitosa ndani mwake bila ratiba wala mpangilio ila ni kosa kubwa sana endapo mapenzi haya yatamwacha yeyote yule akiwa na mengi ya kuwaza na bila amani.

Mwisho, ni vyema kuteleza. Kuteleza huambatana na mafunzo bora maishani. Tusiwakemee wala kuwacheka wale ambao wameteleza! Tuwasaidie na tuwape nafasi nyingine.

Facebook: Stephen N Mburu

Twitter: MwandishiMburu

 

Share this story
Pastor Burale: Having a side chick does not relieve stress
Alcohol has never solved any problem. True, alcohol can be used for relaxation and entertainment.
Love triangle leaves cop, girlfriend dead, wife widowed
Wife says he was a respectful man who sought forgiveness whenever he made mistakes.
.
RECOMMENDED NEWS
Feedback