Skip to main content
× THE NAIROBIAN POLITICS TEN THINGS ASIAN ARENA TRAVEL FEATURES NAIROBIAN SHOP MONEY FASHION FLASH BACK HEALTH UNCLE TED BETTING Podcasts E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×
SPORTS

Jamani, Usipate ball juu ya msimu wa baridi

BLOGS
By Stephen Mburu | July 15th 2021

Baridi ya mzizimo inapiga kulia na kushoto. Baridi hii inawafanya wanaume kwa wanawake kujikunyata kila sehemu. Hata wanavyotembea imekuwa tofauti.

Kila kundi la watu limekuwa likionyesha jinsi baridi hii imewaathiri; si wakulima, si waalimu shuleni na pia wanafanyabiashara. Kila mtu anaumia popote pale alipo kwani wateja hawafiki wakati unaotarajiwa.

Kibaya zaidi ni kwamba kuna curfew! Lakini je, tumeangalia manufaa ya baridi hii maishani mwetu? Je, tumeangazia manufaa yanayotokana na hali hii ya anga ambayo imewaacha wengi wanalia na kusononeka?

Kwanza kabisa, msimu wa baridi ni bora kwa wanafunzi. Wanafunzi hupata fursa ya kusoma kwa utulivu bila kutatizwa na joto jingi ambalo huwatatiza wakati wao wa kudurusu.

Kando na ya masomoni, tuwaze kuhusu manufaa ya baridi hii shadidi katika mahusiano ya kimapenzi. Najua ushaelekea kwingine, ila nitakurejesha kule kufaako.

Nchi ambayo tumezoea kuskia mambo tele bila kuogopa ni vyema kujua kwamba baada ya kila mmoja kurejea kwake kutoka Naivaisha kutazama na kufurahia mashindano ya Safari Rally, sasa kila mmoja anazungumzia kuhusu baridi hii.

Kwa wapenzi wanaopenda kugombana kila baada ya dakika kumi, msimu huu unawasaidia si kutuliza ubishi na ugomvi wao bali wanatafuta angalau sababu ya kutoona makosa kwa wenzio.

Si hilo tu bali pia wakati huu wanautumia vyema kufika manyumbani mapema ili wapate muda wa kujituliza ubongo na badala ya kuzua rabsha wanatumia muda huu kuwajulia hali wapenzi wao.

Kwa mfano, ukiishi na jirani anayependa kurusha cheche za maneno kwa mkewe utagundua kwamba wakati huu amenywea. Amenyamaza ji! Kama maji mtungini. Hasemi chochote, haambi lolote.

Yaani yeye hasikiki. Anafika nyumbani mapema. Anakaa na wanawe na kuwasaidia kufanya homework huku akingoja angalau atengenezewe kikombe cha chai anywe ahisi joto.

Kwa wengi najua hili wanaiona msimu huu wa baridi tu. Ikaisha nao wema, utulivu na ukomavu wa wapenzi wao utakuwa umeisha. Angalau twafaa kushukuru baridi hii kwa kazi nzuri!

Vile vile, wapenzi wanafaa kutumia muda huu kujuana zaidi ya vile wanavyojuana. Wanafaa kutumia kila sekunde kwa kuhakikisha kwamba wanafunzana na kuelezana kuhusu yale mambo ambayo wanayapenda sana.

Si hilo tu bali pia, wanafaa kutumia muda huu kujipanga kuhusu siku za usoni. Wanafaa kutumia muda huu kwa kujadiliana kuhusu kesho ya familia yao na jinsi watakavyowekeza ili wasipate masaibu yanayoweza kuepukika.

Kwa vijana ambao bado hawajawaza kuhusu watakayeoa na watakaye olewa naye, huu si muda wa kuchovya buyu la asali. Kamwe huu si wakati wa kujaribu kuzamia mambo ambayo hamjayapangia.

Wakati mwingi maishani huwa tunajipata katika nafasi zingine kutokana na kutojipanga vyema. Huwa tunajikubali jinsi tulivyo kwa kusema kwamba “Mambo ya kesho yatajipanga tu!”

Hii ni mojawapo ya kauli ambazo huwa inaangamiza si vijana tu bali pia watu wenye umri wa makamu. Hali ya kujiachilia tu na kungoja kesho ambayo hatujaipangia.

Kwa vijana wa kiume ambao wanatumia muda huu kujaribu iwapo mistari yao inaweza kuwasaidia kunasa mabinti, juane kwamba huu si wakati wa kutenda hilo. Mtajipata pabaya kiasi cha kwamba hamtaweza kujinasua.

Vile vile, msijaribu kukaribie mabinti bila mipango. Makinikeni kujipata katika mitego ambayo ilisababishwa na mambo ya msimu kama baridi.

Kwa mabinti ambao wanapania kutumia fursa hii kuwanasa wanaume ili wavune ambako hawakupanda wajue kwamba hata mwizi aliyepatikana akishika mbuzi wa jirani tayari kukimbia naye atadai kwamba hata hajawahi mwona mbuzi mwenyewe.

Jituzeni na heshima mtapata bila kubidiika. La msingi na mwisho ni kwamba baridi hii ya msimu isitufanye tuishi ndivyo sivyo. Tuishi tukijua kwamba wakati wa jua kali ukifika tutaweza kufurahia ukomavu wetu. Tusiwe watu wa misimu! Wanatafakari hoiyee!

Facebook: Stephen N Mburu

Twitter: MwandishiMburu

Share this story
How the rich and famous mourn their pets
Depending on an individual’s ability to cope with loss, some will need psychological support.
I made Sh400,000 grooming the dead
Because of the dead, I’m now a journalist and a happily married father-of-two
.
RECOMMENDED NEWS
Feedback