Watu sita Wauwawa na Wanamgambo wa Al Shabaab Eneo la Elwak

News

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, WATU sita wameuliwa na wanamgambo wa Al Shabaab kuyavamia mabasi mbili eneo la Elwak, Kaunti ya Mandera.

Shambulizi hilo limetekelezwa kati ya miji ya Wargadud na Elwak baada ya wanamgambo hao kuyamininia risasi magari hayo katika kituo cha Corner S mwendo wa saa nne asubuhi.

Kamanda wa eneo la kaskazini mashariki Mohamed Saleh amesema kuwa watu sita akiwemo polisi wa akiba waliuliwa kwenye shambulizi hilo huku wengine wakiwachwa na majeraha.

Inaarifiwa kuwa mabasi hayo yalikuwa chini ya ulinzi wa polisi yaliposhambuliwa.

Ni jana ambapo Kaimu Naibu wa Kamishna wa Mandera Mashariki Yonah Nyawir alitangaza kupigwa  marufuku kwa usafiri wa wageni wanaoingia au kuondoka kaunti hiyo kwa basi hadi mfungo wa Ramadhan uishe.

Kwa mujibu wa kamati ya Usalama ya Kaunti hiyo, wasafiri wanaotumia basi mara nyingi hushambuliwa na makundi ya kigaidi.

Athletics
Dancing queen Mary Moraa retains her 800m title at Kip Keino Classic, Tebogo and Lindsey tie
Athletics
Kibet leaves room for improvement after good show in 5000m at Kip Keino Classic
Athletics
Were takes Nyayo by storm with meet record at Kip Keino Classic as Chelimo wins silver in 5000m
Football
FKF-PL: No love lost as Gor Mahia, AFC Leopards face off in Mashemeji Derby