Rais Kenyatta na Naibu wa Rais William Ruto waendelea kujibizana vikali

Zikiwa zimesalia siku 7 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, cheche kali za kisiasa zimeendelea kushuhudiwa baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuhusu uchaguzi mkuu wa Agotsi 9.

Akizungumza Jumapili wakati wa ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nairobi Express Way, Kenyatta amemtaka Ruto kufanya kampeni zake bila kulitaja jina lake, akisema Wakenya ndio watakaoamua.

Kauli ya Kenyatta inafuatia madai ya Ruto kwamba Kenyatta anawatumia machifu kufanikisha ushindi wa mpinzani wake Raila Odinga.

Haya yanajiri huku mrengo wa Azimio ukiyaingilia malumbano baina ya wawili hao.

Licha ya Kenyatta kumjibu Ruto kuhusu madai ya kumtishia maisha, mgombea mwenza wa Azimio Martha Karua amemtaka Ruto kuandikisha taarifa kwa polisi iwapo ana uhakika kuhusu madai hayo.

Akizungumza mjini Eldoret, Karua amesema madai hayo hayapaswi kutolewa siku chache tu kabla ya uchaguzi wiki mkuu.

Mrengo wa Kenya Kwanza Jumapili ulifanya kampeni kwenye maeneo ya Kaunti za Nandi, Vihiga na Trans Nzoia huku Azimio ikifanya kampeni kwenye Kaunti za Nandi na Uasin Gishu.

Katika mapeni zake, Kenya Kwanza ilisisitiza haja ya Wakenya kujitokeza kwa wingi ili kumchagua Ruto. Musalia Mudavadi ni kigogo mwenza wa Kenya Kwanza.

Boxing
Andiego eyes Olympics slot after victory at Nelson Mandela Cup
Football
FKF-PL: Are fans back to the stadiums or it is false hopes?
By AFP 23 hrs ago
Football
Bellingham brings Real Madrid to brink of La Liga title with Clasico winner
By AFP 1 day ago
Football
It's Man United verses Man City in FA Cup final