Shule zote nchini zitafungwa kwa muda kuanzia tarehe 6 mwezi Agosti ili kupisha shughuli ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.
Akizungumza katika Shule ya Upili ya Alliance, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema shule zitafungwa kwa siku 9 hadi Agosti tarehe 15 kwa kuwa nyingi zinatumika kama vituo vya kupigia kura.
Hata hivyo amesema iwapo kutafanyika duru ya pili ya uchaguzi wa basi shule zitasalia kufungwa hadi ikamiike. Amesema maandalizi ya mitihani ya kitaifa ambayo imeratibiwa kufanyika Novemba mwaka huu yanaendelea akisema iwapo shughuli za masomo zitaathirika sana na uchaguzi mkuu, basi washikadau katika sekta ya elimu watafanya jadiliano iwapo mitihani hiyo itafanyika au itaahirishwa.
Ikumbukwe kulingana na kalena ya masomo ya mwaka huu shule zinatarajiwa tena kufungwa kati ya 17 mwezi septemba hadi tarehe 25 mwezi huo kwa kipindi cha wiki moja. Muhula wa tatu unatarajiwa kuanza Septembe 26 hadi novemba 28 ambapo zitafungwa kupisha mitihani ya kitaifa ya Darasa la nane KCPE na Kidato cha Nne KCSE.