Premium

Wafula Chebukati amaesema huenda wakaahirisha uchaguzi katika baadhi ya maeneo

Huenda  IEBC ikalazimika kuahirisha uchaguzi katika maeneo ambayo yanakumbwa na mivutano baina yake na wawaniaji wa nyadhfa za kisiasa.

Akizungumza mapema leo hii katika mkutano baina ya Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa NCIC na Mkenya Daima, Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, amesema iwapo kesi zilizo mahakamani hazitaamuliwa mapema basi itabidi uchaguzi katika maeneo hayo ufanyike baada ya Agosti 9.

Amesema tayari uchapishaji wa karatasi za kupigia kura imeanza na shughuli nzima ya uchaguzi haiwezi kuahirishwa kutokana na maeneo machache tu yanayokumbwa na utata.

Ikumbukwe shehena ya kwanza ya karatasi hizo iliwasili nchini Alhamisi wiki hii huku ile ya mwisho itakayojumuisha karatasi za kupigia kura za urais ikitarajiwa nchini, tarehe 29, mwezi huu.

Baadhi ya maeneo hayo ni Nairobi ambapo kuna mvutano kuhusu mwaniaji wa kiti cha Uugavana Johnson Sakaja, wa UDA kuhusu uhalali wa cheti chake. Mahakama ya Nairobi inatarajiwa kutoa uamuzi Jumatatu ijayo. Eneo jingine ni Mombasa ambapo mwaniaji wa Ugavana Mike Sonko aliwasilisha kesi mahakamani kulalamikia hatua ya IEBC kukataa kumuidhinisha kwa sababu alibanduliwa mamlakani akiwa Gavana wa Nairobi.

Sonko anataka ajumuishwe miongoni mwa wawaniaji wa ugavana Mombasa. Kwa mara nyingine ameitetea tume hiyo kifuatia madai ya kuwapo makamishna wenye miegemeo ya kisiasa.

Volleyball and Handball
Chumba back as KCB aim to reclaim continental title in Cairo
By AFP 1 day ago
Sports
Kenya's Munyao gets better of Bekele to win London Marathon
By AFP 1 day ago
Football
Arsenal thrash Chelsea 5-0 to open up Premier League lead
By AFP 1 day ago
Football
Inter Milan seal Scudetto in derby thriller with AC Milan