Thika Queens yavizia taji la Ligi Kuu

By Mohammed Awal: Friday, February 21st 2020 at 12:01 GMT +3 | Football
Mchezaji wa Thika Queens akiwania mpira na mchezaji wa Vihiga Queens.[Jonah Onyango Standard]

Klabu ya kina dada Thika Queens imeweka wazi azma yake ya kuwania taji la Ligi ya kina dada msimu huu mpya unapoanza.

Malkia wa Thika watakuwa wageni wa Gaspo F.C mahasimu wao wa jadi katika uga wa Ruiru kaunti ya Kiambu.

Mechi hii ya kufaana itakuwa mtihani wa kwanza kwa malkia hao wa Thika, fumbo ambalo kocha wao Granton Mganga anaamini ataifumbua kwa urahisi.

Kikweli mechi hiyo ni debi ya hapa nyumbani, tunatarajia upinzani mkali, lakini ninaimani, ndaweza kupata ushindi” Mganga alisema.

Msimu uliopita, wanadada hawa wa Thika waliambulia nafasi ya tatu nyuma ya Gaspo F.C na mabingwa mara tatu kwa mpigo Vihiga Queens.

Vihiga queens ilitamba msimu uliopita kwa uweledi wao wa ushambuliaji huku wakitoa mfungaji bora wa msimu jana Terry Eshienga aliyetia kimyani mabao 36.

To get the latest soccer news, text 'SPORTS' to 22840.

Uweledi huu wa Vihiga Queens ndio unaomtia joto nahodha wa Thika Lucy Gladys ambaye anawaona kina dada wa kaunti ya Vihiga kama tishio katika azma yao ya kubeba taji msimu huu.

“Timu itakayotutatiza ni vihiga, msimu jana tuliweza kupata sare na wao, sioni timu nyengine itakayotusumbua msimu huu,” Gladys alisema.

Baada ya Harambee Starlets kung’ara na kuchukua ubingwa wa CECAFA, wachezaji wa vilabu vya humu nchini, walipata nafasi za uhamisho kuenda kuchezea vilabu vingine ughaibuni.

Ngome ya malkia wa Thika haikusazwa katika uhamisho huu, huku malkia hao wakitarajia kumpoteza mshambuliaji wao hodari Mwanalima Adam ambaye ameviziwa na klabu ya Uswidi.

Malkia hao wanaimani, wataweza kuifunga pengo lake Mwanalima na hawatakosa makali mbele ya goli.

“Licha ya kuwa huenda tukampoteza mshambuliaji wetu Mwanalima Adam klabu tayari tumepata ufundi wa wachezaji wengine wapya watakao ziba pengo hilo” nahodha Gladys alidokeza.

Msimu mpya wa Ligi kuu ya wanawake humu nchini inatarajia kuanza 22 Jumamosi  huku jumla ya mechi nane zikitarajiwa kugaragazwa.

  1. Gaspo fc vs thika queens ( ruiru stadium)
  2. Oserian ladies vs kahawa queens ( oserian grounds)
  3. Kayole starlets vs zetech spartans ( stima members club)
  4. Sep oyugis vs kibera girls ( k’otieno)
  5. Mathare united vs nakuru west queens ( camp toyoyo grounds)
  6. Wadadia vs eldoret falcons ( mumias sports complex)
  7. Trans nzoia falcons vs vihiga queens ( manour stadium)
  8. Kisumu all starlets vs makolanders ( moi stadium)

For More of This and Other Sports Stories Subscribe to the Standard Epaper

LATEST STORIES
POPULAR HEADLINES