Mulumba avunja ndoa yake ya miaka mitano na Bandari

By Mohammed Awal: Friday, February 14th 2020 at 10:40 GMT +3 | Football
Felly Mulumba akiwa na kocha wa klabu yake mpya Henrik Pieter de Jong  Fc Platnum.Picha [Hisani]

Klabu ya bandari imempoteza nahodha wao Felly Mulumba aliyegura klabu hio kuelekea nchini zimbabwe kuichezea klabu ya Platnum.

Mulumba mwenye asili ya Congo ametia saini mkataba wa miaka miwili na klabu yake mpya jijini Harare.

Klabu ya Bandari kupitia mtandao wao wa twita imemshukuru nahodha wao wa zamani na kumtakia kila la heri katika klabu yake mpya.

Kuondoka kwake ni pigo kwa klabu hiyo kwa sasa huku Bandari ikiweza kunakili ushindi mara tano tuu msimu huu, wakipoteza mechi tisa na kutoka sare mechi tano, matokeo yanayowacha katika nafasi ya 11 na pointi 20.

Mulumba akizungumza kupitia akaunti yake ya Facebook, ameishukuru usimamizi kwa klabu ya Bandari, wachezaji wenzake na mashabiki wa timu hiyo.

To get the latest soccer news, text 'SPORTS' to 22840.

Mulumba amebeba mataji matatu kwa kipindi cha miaka mitano aliyoichezea klabu ya Bandari na kuisaidia timu hiyo ya pwani kuibuka nambari ya pili katika Ligi Kuu nchini nyuma ya mabingwa Gor Mahia.

Klabu ya Platinum itakuwa klabu yake ya tano kwa beki huyo, hapo nyuma amewai kuigaragazia klabu ya As Saint Luc nchini Congo, na klabu za Posta Rangers, Sofaka na Bandari humu nchini.

Hivi majuzi kumekuwa na tetesi kuwa vilabu vingine vimekuwa vikiwa mezea mate wachezaji wa bandari William Wadri na Hassan Abdalla na huenda uhamaji huu ukawa ndio mwanzo tuu wa wachezaji kuondoka bandarini.

For More of This and Other Sports Stories Subscribe to the Standard Epaper

LATEST STORIES
POPULAR HEADLINES
Beach Volleyball: Coach Mulinge drops two
Beach Volleyball: Coach Mulinge drops two
Volleyball and Handball 2 days ago