Mvumilivu hula mbivu: Harambee Stars hoyeee!

Wachezaji wa Harambee Stars wakumbatiana baada ya kufunga bao [STANDARD]

Kila jambo jema huwa na mwanzo mgumu tena wenye nuksi na kukorofishana ikibidi! Ingawa hivyo, mwisho wake huwa mtamu kama haluwa. Ndio hapo waambiwa cha jasho hakikosi utamu. Yaani kwa kifupi, mvumilivu hula mbivu.

Nianze kwa kusema kuwa leo hii jarida hili linaivulia kofia timu ya taifa ya soka Harambee Stars. Wanavyosema watu: twaizimia timu ya soka nchini sigareti.

Nakumbuka papa hapa kwenye jarida hili tukiwahongera dada zetu kwa maana ya Starlets baada ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika. Tukawa tunawabeza sana maghulamu, yaani Harambee Stars. Kumbe?

Hali iko vipi. Wakenya wanasubiri kujua hatima ya Siera Leone kabla ya kuanza kupiga mbinja. Hadi ninapoyaandika makala haya, Kenya ilikuwa inaoliongoza kundi la F ambalo pia linajumuisha mataiafa ya Ghana, Ethiopia na Siera Leone.

Kuna zahama za kupambana na ufisadi nchini Siera Leone ambazo zimefanya serikali ya nchini humo kumpiga panga rais wa soka nchini humo na katibu wake kutokana na madai ya ufisadi na upangaji wa matokeo.

Hilo lina maana kuwa shirikisho la soka duniani FIFA huwa halikubali serikali yoyote ile kuingilia usimamizi wa soka nchini mwake. Ikabidi FIFA kuipiga marufuku ya soka nchi ya Siera Leone. Ndio maana nchi hiyo haikucheza wiki iliyopita mechi mbili ya ugenini na nyumbani dhidi ya Ghana. Haya yametufika pia nasi Wakenya!

Hivyo basi, matokeo ya Siera Leone yakifutiliwa mbali, ina maana kuwa ushindi wa Ethiopia dhidi ya Siera Leone ambapo Ethiopia ilishinda bao moja kavu, kisha yiyo hiyo Siera Leona ikailaza Kenya mawili kwa moja pia matokeo hayo yafutiliwe mbali.

Wachezaji wa Harambee Stars watazama uwanja kabla ya mechi dhidi ya Ethiopia [STANDARD]

Yote hayo tisa, kwa kuwa Ghana itapewa ushindi wa mechi mbili dhidi ya Ethiopia ambazo hazikuchezwa, basi Ghana na Kenya ndizo nchi zitakazofuzu kutoka kundi la F. Na kama Siera Leone itasamehewa, itabidi Kenya ipate tu sare hapa nyumbani dhidi ya nchi hiyo ili kufuzu.

Kwa kifupi twaweza kusema kuwa baada ya mechi nne, guu moja la Kenya lipo katika fainali za Afrika nchini Cameroon mwakani mwezi Januari.

Mara ya mwisho Kenya imefuzu AFCON ilikuwa mwaka 2004. Ulikuwa wapi jamani msomaji wangu? Ni kitamboje? Nahodha alikuwa Musa Otieno. Rais alikuwa Mwai Kibaki. Mkate ulikuwa wauzwa shilingi kumi! Ni kitambo jamani!

Majuzi kabla ya mchuano huo wa uwanjani Kasarani ambapo Kenya iliidengua Ethiopia, waziri wa Michezo Rashid Echesa aliamuru kiingilio kiwe bure bwerere. Yaani macho tu. Na uwanja ulijaa kweli!

Naibu rais William Ruto akaahidi basi. Timu ya taifa haina basi jamani! Imagine!

Kwa sasa twasubiri kima cha shilingi milioni hamsini kutoka kwa ndugu William Ruto! Lakini twasubiri tu kujua hatima ya Siera Leone!

Mbona lakini serikali ina mazoea ya kuzichangamkia timu za kitaifa wakati zimefika mlangoni na mtungi? Iweje serikali zetu hasa wizara ya michezo kuzibaa, kuja kutahamaki wakati kumepamzazuka! Twatafuta blanketi wakati kumekucha jamani!

Hongera tena Harambee Stars!

Hassan mwana wa Ali ni Mhariri wa Michezo na Nahodha wa Nuruyalugha (RADIO MAISHA).

[email protected], [email protected], FB: Ali Hassan Kauleni, Hassan mwana wa Ali,

Twitter: @alikauleni

Athletics
Kenyan stars ready for World Cross showdown in Belgrade
By Ben Ahenda 3 hrs ago
Motorsport
Safari Rally 2024: Tanak urges Kenyan children to take up motorsports as a career
Rugby
SCHOOLS: From the classroom to the field, Kisumu Girls ready to lift national rugby trophy
Motorsport
Safari Rally 2024: Neuville clinches Kasarani stage as Hyundai makes intention known