×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenyatta aongoza maadhimisho ya 58 ya Jamhuri

Kenyatta aongoza maadhimisho ya 58 ya Jamhuri

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuliongoza taifa kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya Siku ya Jamuhuri katika Bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi.

Jumla ya watu 10,000 wanahudhuria maadhimisho hayo ikiwa njia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona.

Maadhimisho hayo ni ya mwisho chini ya uongozi wa Kenyatta ambaye atastaafu mwaka ujao.

Kinyume na ilivyofanyika mwaka wa 2013 miezi michache tu baada ya kuapishwa kuwa rais na kuongoza Jamhuri ya kwanza chini ya uongozi wake, Rais alitoa ahadi  mbalimbali, na kupigia debe Katiba ya mwaka wa 2010 na kuahidi kutekelezwa kwake, tofauti na sasa ambapo Kenyatta amekuwa mmoja wa wale ambao wanashinikiza katiba  hiyo kufanyiwa marekebisho.

Aidha, Rais ataweka bayana hatua ambazo zimepigwa na serikali yake katika nyanja mbalimbali hasa katika kulinda Uhuru wa taifa na kufanikisha maendeleo kwaajili ya mamilioni ya Wakenya.

Aidha, Siku ya Jamhuri inafanyika taifa likiwa tayari limeingia katika siasa za mwaka ujao, Rais alikioneka kuunga mkono mrengo wa Kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Siku hii huadhimishwa kila tarehe 12 mwezi  Desemba kukumbuka siku ambayo Kenya ilijipatia Uhuru kutoka mikononi mwa mabeberu mnamo mwaka wa 1963.

Kama ilivyo ada,siku hii haiwezi kukamilika bila kutajwa kwa majina ya mashujaa sita waliopigania uhuru wa nchi maarufu the Kapenguria Six, Mzee Jomo Kenyatta, Kun'gu Karumba, Bildad Kagia, Achieng' Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai.

Aidha mashujaa wa ukombozi wa pili wa nchi mfano Ronald Ngala  kamwe hawawezi kusahaulika.

Siku iliyotangulia, Rais alizindua sanamu ya Ronald Ngala jijini Nairobi kama ishara ya kukumbuka mchango wake katika kupigania ukombozi wa Kenya.

Share this: