×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tangazo la Raila kuwania urais ni la kawaida tu; wasema wandani wa Ruto

Tangazo la Raila kuwania urais ni la kawaida tu; wasema wandani wa Ruto

Wandani wa Naibu wa Rais, William Ruto wameendelea kupuuza tangazo la Kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwania urais mwaka ujao.

Wakizungumza kwenye sherehe ya kitamaduni ya Jamii ya Turkana, maarufu Tobong'u Lore, viongozi hao wametaja tangazo hilo kuwa  la kawaida tu na kwamba si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuwania urais.

Aidha, wamesema ni usaliti kwa Rais Kenyatta na baadhi ya Vigogo wa One Kenya Alliance, OKA kukosa kuhudhuria hafla hiyo ya Azimio la Umoja ambapo Odinga alitangaza azma ya kuwania urais.

Aden Duale ni Mbunge wa Garissa Mjini.

Kwa upande wake Naibu wa Rais William Ruto ameendelea kumsuta Odinga kwa madai ya kuwahadaa Wakenya.

Kwa mara nyingine Ruto amepuuza uwezo wa watu wachcahe wenye ushawishi nchini maarufu System, akikariri kwamba hawana nguvu za kuamua atakayekuwa rais na kwamba wananchi wa kawaida ndio watakaomchagua rais.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Gavana wa Turkana Josphat Nanok.

Viongozi walioandamana na Ruto akiwamo Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago wameendelea kupigia debe azma yake ya kuwa rais mwaka ujao.

Sherehe hiyo Tobong'uLore imehudhuriwa na viongozi mbalimbali na hufanywa kila mwaka kusherehekea amani kati ya Wa-Turkana na jamii za mataifa yanayopakana na kaunti hiyo ya Turkana kama vile Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia.

Share this: