×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Afisa wa polisi ajiua, Elgeyo Marakwet

Afisa wa polisi ajiua, Elgeyo Marakwet

Katika kisa cha kuhuzunisha,

Afisa mmoja wa polisi katika eneo la Emkoin Kkwenye Kaunti ya Uasin Gishu amejiua kwa kujiteketeza.

Maafisa wenzake walioshuhudia kisa hicho, wanasema afisa huyo Wa cheo cha Inspekta, Sammy Chirchir alijifungia ndani ya nyumba kisha kuwasha moto.

Majirani wanasema walifika nyumbani kwa afisa huyo walipoona moshi mkubwa, na kwamba walimpata mwanawe akiwa nje, ambaye aliwaarifu kwamba baba yake alikuwa akiteketeza godoro ili kuwafukuza nyuki waliokuwa wameingia katika nyumba yao.

Wanasema afisa huyo wa polisi alikataa kufungua mlango walipofika kumwokoa, na kwamba alikuwa ameufunga kwa upande wa ndani.

Iliwalazimu kuwaita maafisa wa Idara ya Kuzima moto , ambao walifika na kumpata afisa huyo akiwa tayari amefariki dunia licha ya kufanikiwa kuuzima moto huo.

Mke na mtoto mwingine wa marehemu afisa huyo wa polisi, hawakuwa nyumbani wakati kisa hicho kilipotokea huku majirani wakisema marehemu alikuwa ameanza hulka ya unywaji pombe kupita kiasi.

Pia, wamesema alikuwa akilalamikia kuhamishwahamishwa kila mara.


Polisi huyo ambaye ni baba wa watoto wawili, alikuwa akifanya kazi mjini Lodwar baada ya kuwahi kuwa katika kituo cha Polisi cha Huruma mjini Eldoret kabla ya kuhamishiwa Turkana

Kamanda wa Polisi wa Eneo la Turbo Edward Masibo amesema bado sababu maalumu ya afisa huyo kujiua haijabainika na kwamba tayari uchunguzi umeanzishwa.

Huyu ni afisa wa tatu kujiua wiki hii pekee, ambapo Alhamisi Usiku  polisi alijiua  katika Kaunti ya Mombasa na kuacha barua yenye maelezo kuhusu yale ambayo alitarajia kufanyiwa baada ya kufariki dunia.

Aidha Jumanne wiki hii, afisa kwa jina Benson Imbatu aliwaua watu sita akiwamo mpenzi wake kabla ya kujiua katika eneo la Kangemi hapa Nairobi.

Share this: