×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hatumpingi Odinga katika OKA, tuko pamoja, Moi asema

Hatumpingi Odinga katika OKA, tuko pamoja, Moi asema

Kiongozi wa KANU, Gedion Moi ambaye ni mmoja wa vigogo wa muungano wa One Kenya Alliance OKA, amesifu ukakamavu wa Kiongozi wa ODM Raila Odinga akisema OKA haimpingi Raila na kwamba filosofia na lengo lao ni moja.

Moi alikuwa akimjibu Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU, Francis Atwoli, ambaye katika hafla ya Azimio la Umoja katika Uwanja wa Kasarani, alimhimiza Moi kujiondoa kutoka OKA ili kuungana na mrengo wa Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Wakati wa hafla hiyo, sauti za viongozi mbalimbali zilichezwa kurejelea misururu ya mikutano ya Odinga, ambapo alikutana na makundi ya watu tofauti tofauti, kisha kupokea maazimio ya masuala ambayo wangependa ayashaghulikie iwapo atakuwa Rais.

Baadhi ya viongozi hao akiwamo Seneta wa Siaya, James Orengo, waliwakashifu vigogo wa kisiasa ambao wanapinga azma ya Odinga, wakisema si lazima Rais ashirikiane na wanasiasa wanaoweka vikwazo vya kutaka ahadi za kugawana mamlaka.

Ikumbukwe Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa FORD Kenya wamekosa kuhudhuria licha ya kualikwa wakisema wana shughuli za binafsi, huku Kalonzo Musyoka wa Wiper akiwa Sudan.

Share this: