×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Niko kwa debe, Raila ajitosa katika kivumbi cha 2022

Niko kwa debe, Raila ajitosa katika kivumbi cha 2022

Hatimaye Kiongozi wa ODM, Raila Odinga amejitosa rasmi katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2022.

Raila ametoa tangazo hilo katika hafla ya kipekee ya Azimio la Umoja katika Uwanja wa Kasarani, Nairobi.

Aidha, Raila ametumia fursa hiyo kudokeza kuhusu mambo atakayoyafanya kipaumbele huku magavana, mawaziri na viongozi wakuu serikalini wakijumuika na maelfu Wakenya.

Kwa tangazo hilo, Raila aliwasisimua kadhalika kuwaridhisha maelfu ya Wakenya waliojumuika uwanjani Kasarani kuanzia jana usiku wote wakiwa na matarajio yayo hayo.

Na kwa njia ya kipekee, aliyekuwa Spika Francis Ole Kaparo aliwasilisha matamanio hayo ya Wakenya kwa njia ya mswada uliosomwa na Mkenya, Victor Njoka.

Kadhalika, mkewe Raila Odinga alikuwa radhi kumwacha tena muewe kuzamia kampeni za urais kwa mara ya tano sasa.

Katika hotuba yake, Raila ameorodhesha baadhi ya suluhu anazopendekeza ili kuwasaidia Wakenya baada ya kuwasilikiliza Wakenya kote nchini. Miongoni mwa mikakati hiyo ni mpango wa Inua Jamii.

Pia amependekeza mpango wa matibabu kwa jina BabaCare.

Mapendekezo mengine ni kama vile Kazi kwa wote na uchumi kwa kina mama.

Vilevile ana mipango ya kukuza matumizi ya dijitali, elimu kwa wote, fukuza njaa na one county one product. Magavana takriban 30, mawaziri na makatibu wa serikali ni miongoni mwa waliohudhuria.

Hafla hiyo pia ilitawaliwa na mbwembwe, burudani, kauli za kusisimua na za kuvunja mbavu.

Share this: