×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

EACC yapiga hatua katika vita dhidi ya ufisadi

EACC yapiga hatua katika vita dhidi ya ufisadi

Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC imeongoza hafla ya Siku ya Kimataifa ya Kukabili Ufisadi kwenye Bustani ya Mama Ngina jijini Mombasa kaulimbinu ya mwaka huu ikiwa ni Haki Yako Jukumu Lako, Kataa Ufisadi, kwa Kiingereza - Your Right Your Role, Say No to Corruption.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Twalib Mbarak ametaja utepetevu miongoni mwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mashtaka ya Umma pamoja na Idara ya Mahakama kuchangia baadhi ya kesi za ufisadi kutupiliwa mbali.Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu Kihara Kariuki amesema idara yake imeweka mikakati ya kuzuia ufisadi katika ofisi mbalimbali za serikali.

Ametaja suala la maafisa wakuu serikalini kufanyiwa ukaguzi wa mtindo wa maisha pia kuchangia kukabiliwa kwa sakata mbalimbali za ufisadi ambazo wamekuwa wakihusishwa nazo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma, ODPP amewahimiza Wakenya kuhakikisha wanawachagua viongozi wanaofaa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa Haji, viongozi wafisadi wamekuwa wakihujumu utendakazi wa idara mbalimbali zinazopiga vita ufisadi.

Mwaka wa 2013, Umoja wa Mataifa ulitenga tarehe 9 Disemba kuwa Siku ya Kukabili Ufisadi.

Share this: