×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta aanza rasmi ziara ya siku tatu Tanzania

Rais Kenyatta aanza rasmi ziara ya siku tatu Tanzania

Rais Uhuru Kenyatta ameanza rasmi ziara ya siku tatu nchini Tanzania.

Kenyatta aliyewasili leo nchini humo, ameahudhuria maadhimisho ya miaka sitini ya uhuru wa taifa la Tanzania jijini Dar es Salaam.

Rais ambaye amekuwa mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo alialikwa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu kusherehekea hatua ambazo zimepigwa na Tanzania kwa kipindi cha miaka sitini tangu ipate uhuru.

Akihutubu wakati wa hafla hiyo, Rais Samia amesema ziara ya Kenyatta ni muhimu katika kuonesha urafiki na ushiriakiano kwani itakuwa ya mwisho katika hatamu yake ya uongozi akielekea kustaafu mwaka ujao.

Kulingana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Daniel Kazungu, Kenyatta ameratibiwa kutia saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano hapo kesho.

Kenya na Tanzania zimekuwa zikishirikiana tangu Samia alipochukua hatamu ya uongozi kufuatia kifo cha Hayati John Pombe Magufuli.

Share this: