×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sibabaishwi na Azimio la Umoja, asema Ruto

Sibabaishwi na Azimio la Umoja, asema Ruto

Naibu wa Rais, William Ruto amesisitiza kwamba hababaishwi na hatua ya baadhi ya mabwanyenye kuunga mkono azma ya Kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwa Rais mwaka ujao.

Akihutubu katika Kaunti ya Makueni, Ruto ambaye amekuwa akizuru eneo la Ukambani mara kwa mara akiwahimiza wakazi kumuunga mkono amerejelea kauli yake kwamba mabwanyenye hao wanafanya hivyo kulinda tu mali zao wala si kwa kuwajali wananchi.

Aidha, Ruto amedai kwamba Odinga yu katika njiapanda hasa ikizingatiwa vigogo wa One Kenya Alliance, OKA akiwamo Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi wamekataa kumuunga mkono.

Ruto ameandamana na viongozi mbalimbali wa eneo hilo la Ukambani.

Share this: