×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maandalizi ya Azimio la Umoja yakamilika Kasarani

Maandalizi ya Azimio la Umoja yakamilika Kasarani

Kiongozi wa ODM, Raila Odinga leo ameandamana na viongozi kadhaa wa chama hicho na washirika wengine wa kisiasa kukagua uwanja wa Kasarani.

Raila ameandamana na Naibu Kiongozi wa ODM Wycliff Oparanya, Gavana wa Kisii, James Ongwae, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed miongoni mwa wengine akiwamo mmliki wa Kampuni ya Royal Media, SK Macharia.

Junet Mohammed amewataka Wakenya kutarajia tangazo kubwa huku maelfu ya wafuasi wakiwa tayari wamewasili jijini kwa ajili ya shughuli hiyo.

Hayo yanajiri huku ikiwa wazi kwamba vinara watatu wa muungano wa OKA hawatahudhuria. Kinara wa ANC, Musalia Mudavadi amesema licha ya kupokea mwaliko, atakuwa na shughuli za binafsi kwa hivyo hataweza kufika japo amemtakia Raila heri.

Kalonzo Musyoka kwa upande wake yuko nchini Sudan Kusini kwa mazungumzo ya amani kupitia wadhifa wake wa kuwa Mjumbe Maalum wa Rais katika taifa hilo. Kiongozi wa FORD Kenya Moses Wetangula vilevile ameasema kwamba hatakuwapo.

Share this: